Thursday, November 18, 2010

ANGALIZO!!

Natumaini u mzima dada yangu, mimi pia. Natarajia kuolewa mwakani mwanzoni tu na nilikua naomba kuuliza, nimepata gauni la harusi but ni off white ila limenikaa vizuri sana napenda kujua wadau hasa kwa sisi wabongo ukivaa off white ni sawa ama ntakua nimechemsha sana? Kwa kweli gauni ni zuri n limenifit ile mbaya kuliko hata meupe niliyoyakuta hapo dukani hofu yangu tu sio jeupe pee, nakuomba uwarushie wadau, put it any how but swali kubwa tu ni kuvaa off white ni sawa kwa culture yetu ya kibongo?????? Mimi ni mkristo. Pia unaweza kunijibu wewe zeze kwa oni lako mpenzi waonaje ili nikalichukue mazima hilo gauni fasta kabla mtu hajaliwahi.

Lightness

"kwa ufahamu wangu mimi kuhusiana na nguo nyeupe na Off white. Eti wanasema kuwa nguo nyeupe pee inatakiwa avae bi harusi ambaye ni bikIra na off white huvaliwa na bi harusi ambaye si bikira, sasa sijui ni maneno mbofo mbofu au la Ila mwisho wa siku najua tunavaa nguo ile tuloipenda....mfano mimi nilivaaga Off white sio kwa ajili ya maneno mbofu mbofu LA HASHA  :) bali tu sikupenda nguo nyeupe pee.so mie nakushauri kama umeipenda na imekukaa vyema go for it!!"

zeze

WADAU MNAMWAMBIAJE?!!

No comments:

Post a Comment